Mikondo ya bahari inafanyaje kazi
-
0:07 - 0:08Mwaka 1992
-
0:08 - 0:12Meli ya mizigo iliyobeba shehena ya Vichezeo vya kuogea ilipatwa na dhoruba.
-
0:12 - 0:15Makontena ya kusafirishia shehena yakapotea kwenye maji,
-
0:15 - 0:21Mawimbi yalisomba bata wa raba na vichezeo vinginevyo kwenye bahari ya Pacific ya kaskazini.
-
0:21 - 0:23Lakini havikukaa pamoja.
-
0:23 - 0:24Tofauti kabisa--
-
0:24 - 0:27Bata hao wametapakaa Dunia nzima,
-
0:27 - 0:30Na wachunguzi wametumia njia yao
-
0:30 - 0:34Kuelewa zaidi mikondo ya Bahari.
-
0:34 - 0:36Mikondo ya bahari inaendeshwa na vitu vingi:
-
0:36 - 0:40Upepo,mawimbi,mabadiliko kwenye wiani,
-
0:40 - 0:43Na mzunguko wa Dunia.
-
0:43 - 0:48Topografia ya sakafu ya bahari na ufukwe vinaongeza hiyo mizunguko,
-
0:48 - 0:49Kusababisha mikondo iongeze spidi,
-
0:49 - 0:52Kupunguza spidi au kubadili muelekeo.
-
0:52 - 0:55Mikondo ya bahari imegawanyika kwenye makundi makuu mawili:
-
0:55 - 0:58Mikondo ya juu na mikondo ya ndani ya bahari.
-
0:58 - 1:00Mikondo ya juu ina dhibiti mwendo
-
1:00 - 1:03Wa asilimia 10 ya maji ya bahari,
-
1:03 - 1:06Wakati mikondo ya ndani inadhibiti asilimia 90 iliyobaki.
-
1:06 - 1:08Japo yanasababishwa na vitu tofauti,
-
1:08 - 1:11Mikondo ya juu na ya ndani inashabiana
-
1:11 - 1:15Ni dansi ambayo inaifanya bahari itembee.
-
1:15 - 1:16Karibu na fukwe,
-
1:16 - 1:20Mikondo ya bahari ya juu inaendeshwa na upepo na mawimbi,
-
1:20 - 1:25Ambayo inavuta Maji ndani na Nje pale ambapo kiwango cha maji kinapungua na kuongezeka.
-
1:25 - 1:30Wakati huo huo,kwenye bahari upepo ndio nguvu kubwa ya mikondo ya juu.
-
1:30 - 1:32Upepo unapovuma juu ya bahari,
-
1:32 - 1:35Unaenda na maji ya juu,
-
1:35 - 1:37Maji yanayotembea yavuta vilivyomo chini,
-
1:37 - 1:40Na hizo zinavuta za chini yake.
-
1:40 - 1:43Maji yenye kina kirefu cha Mita 400
-
1:43 - 1:47Bado yana athiriwa na upepo wa juu ya bahari.
-
1:47 - 1:51Ukiangalia kwa karibu muundo wa mikondo ya juu ya bahari ya Dunia nzima,
-
1:51 - 1:55Utaona kwamba inatengeneza vitanzi vikubwa vinavyoitwa gyre,
-
1:55 - 1:58Inayosafiri upande wa saa kaskazini mwa ulimwengu
-
1:58 - 2:00Na kwa kurudi kusini mwa ulimwengu.
-
2:00 - 2:03Hiyo ni sababu ya jinsi Dunia inavyozunguka
-
2:03 - 2:07Inaingilia muundo wa upepo inayoleta hii mikondo.
-
2:07 - 2:08Kama Dunia isingezunguka,
-
2:08 - 2:11Maji na hewa vingeenda mbele na nyuma
-
2:11 - 2:13Kutoka sehemu yenye presha ndogo ikweta
-
2:13 - 2:15Na presha kubwa kwenye fito.
-
2:15 - 2:16Lakini Kadri Dunia inavyozunguka,
-
2:16 - 2:21Hewa kutoka ikweta kwenda kwenye fito ya kaskazini inageukia mashariki,
-
2:21 - 2:25Na hewa inayoelekea chini inageukia magharibi.
-
2:25 - 2:27Tofauti yake inatokea kwenye ulimwengu wa kusini,
-
2:27 - 2:29Ili kusudi mito mikubwa ya upepo
-
2:29 - 2:33Inatengeneza miundo ya vitanzi karibu na mabonde ya bahari.
-
2:33 - 2:36Hii inaitwa ifekti ya coriolis.
-
2:36 - 2:40Upepo unasukuma bahari chini yake kwenye gyre za kuzunguka.
-
2:40 - 2:44Na sababu maji yanashika moto upesi kushinda hewa,
-
2:44 - 2:48Hii mikondo inasaidia kugawanya joto duniani.
-
2:48 - 2:50Tofauti na mikondo ya juu,
-
2:50 - 2:55Mikondo ya ndani inaendeshwa na tofauti ya wiani wa maji ya bahari.
-
2:55 - 2:57Maji yanavyoelekea fito ya kaskazini,
-
2:57 - 2:58Yanakuwa na baridi.
-
2:58 - 3:01Pia yanakuwa na chumvi nyingi,
-
3:01 - 3:06Sababu ile barafu inayoshikilia maji wakati inaacha chumvi nyuma.
-
3:06 - 3:09Haya Maji ya baridi yenye chumvi ni mazito zaidi
-
3:09 - 3:10Kwahiyo yananuka,
-
3:10 - 3:13Na Maji ya uvugu vugu yanachukua nafasi yake.
-
3:13 - 3:17Kutengeneza mkondo wa wima unaoitwa mzunguko wa thermohaline
-
3:17 - 3:22Mzunguko wa thermohaline wa maji ya ndani na yanayoendeshwa na upepo wa Mkondo wa bahari wa juu
-
3:22 - 3:26Unajiunga kutengeneza kitanzi cha upepo kinachoitwa Global Conveyor Belt.
-
3:26 - 3:29Maji yanavyohama kutoka ndani ya bahari kwenda juu.
-
3:29 - 3:33Yanabeba virutubishi ambavyo vinasaidia kukuza viumbe hai
-
3:33 - 3:36Ambayo inatengeneza msingi wa cheni nyingi za chakula baharini.
-
3:36 - 3:39Mkondo wa Global Conveyor belt ndo mrefu zaidi duniani,
-
3:39 - 3:41Ukizunguka dunia nzima.
-
3:41 - 3:45Lakini unazunguka sentimita chache kwa sekunde.
-
3:45 - 3:49Inaweza ichukua tone la maji miaka 1000 kufanya safari yote.
-
3:49 - 3:53Japokuwa Levo za joto la bahari zinazopanda zinasababisha ukanda wa conveyor
-
3:53 - 3:55Kupunguza spidi.
-
3:55 - 3:58Modeli zinaonesha hii inasabisha ma tatizo kwenye hali ya hewa
-
3:58 - 4:00Kwenye pande zote za Atlantic,
-
4:00 - 4:03Na hamna anayejua nini kitatokea ikiendelea kupunguza spidi
-
4:03 - 4:05Au ikisimama kabisa
-
4:05 - 4:09Njia pekee tutakayoweza tabiri sawasawa na kujiandaa vizuri
-
4:09 - 4:14Ni Kwa kuendelea kusoma mikondo na nguvu zote zinazosababisha mikondo kuwepo.
- Title:
- Mikondo ya bahari inafanyaje kazi
- Speaker:
- Jennifer Verduin
- Description:
-
Mwaka 1992,meli ya mizigo iliyobeba vichezeo ilipatwa na dhoruba. Makontena ya kusafirishia shehena yalipotea kwenye maji, na mawimbi yakasafirisha vichezeo vya bata 28000 na vichezeo vingine mpaka Pacific ya kaskazini. Lakini havikikukaa pamoja -- bata wamesambaa Dunia nzima. Hii ilitokeaje? Jennifer Verduin anaingia kwenye sayansi ya mikondo ya bahari.
Somo limetolewa na Jennifer Verduin, likiongozwa na Cabong Studios.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TED-Ed
- Duration:
- 04:16
![]() |
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for How do ocean currents work? | |
![]() |
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for How do ocean currents work? | |
![]() |
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for How do ocean currents work? |