Maombi nchini Uingereza; Muujiza nchini NORWAY!
-
0:00 - 0:07Nilitarajia. Nilijiambia,
'Kisa hiki kimekaidi maarifa ya matibabu -
0:07 - 0:11na hakitapinga uwezo wa Mungu.'
-
0:18 - 0:25Ikiwa bado kuna maumivu katika sehemu yoyote ya
mwili wako, weka mkono wako hapo. -
0:25 - 0:34Popote pale maumivu hayo yalipo,
katika jina la Yesu Kristo, -
0:34 - 0:37upako wa Roho Mtakatifu
uko hapa kuponya. -
0:37 - 0:47Upone kwa jina la Yesu!
-
0:48 - 0:55Jina langu ni Ivan na ninaishi hapa Norway.
-
0:55 - 0:59Kwa asili, mimi ni natokea Uganda.
-
0:59 - 1:07Nilikuwa na maradhi ambayo
yalinitoa kwenye nafasi yangu. -
1:07 - 1:10Ilibidi hata nichukue wakati wa kupumzika kazini.
-
1:10 - 1:17Na ugonjwa huo ulisababisha
maumivu kwenye kifua changu, -
1:17 - 1:23ambapo nilipata maumivu makali.
-
1:23 - 1:26Sikuweza kueleza
yalikuwa yanatoka wapi. -
1:26 - 1:33yalikuwa makali sana kiasi kwamba
sikuweza kufanya chochote. -
1:33 - 1:37Karibu miaka 15 iliyopita, nilikuwa na
homa ya mapafu kali (acute pneumonia), -
1:37 - 1:41nikiwa bado nyumbani Uganda
kabla sijahamia Norway. -
1:41 - 1:52Na ugonjwa huu ulikuwa mkali sana kwamba sehemu ya
ganda la kushoto la pafu langu iliharibika -
1:52 - 1:56Nililazwa hospitalini kwa mwezi mmoja.
-
1:56 - 1:59Na hata nilipotoka hospitalini,
-
1:59 - 2:05Ilinibidi niwe na kipindi cha kusubiri kupona kidigo kidogo
kwa takriban mwezi mmoja. Ilikuwa mbaya sana. -
2:05 - 2:11Kwa hivyo nilipopata maumivu hayo,
nilianza kiyahusisha na kisa hicho, -
2:11 - 2:17kwamba pengine inaweza kuwa
nimonia ilikuwa inajidhihirisha tena. -
2:17 - 2:21Wakati maumivu yalipoendelea, niliamua ...
-
2:21 - 2:26Kumbuka, wakati huo nilikuwa
nimeacha kufanya kazi kwa sababu sikuweza kugeuka. -
2:26 - 2:34Hata lilipokuja suala la kutembea, kupiga hatua, nilihisi maumivu makali ndani.
-
2:34 - 2:40Hata wakati wowote nilipokuwa nimelala,
nikigeuka kutoka upande mmoja hadi mwingine, -
2:40 - 2:44ilikuwa shida, ilikuwa tatizo.
-
2:44 - 2:48Kwa hiyo niliamua kuwasiliana na daktari wangu.
-
2:48 - 2:53Alipokuwa akinichunguza,
alijaribu kugusa eneo hilo -
2:53 - 2:58kwa sababu nilimwambia kuwa maumivu
yalikuwa ndani ya kifua changu. -
2:58 - 2:59Yalikuwa makali sana.
-
2:59 - 3:03Hata sikujua jinsi
ya kumweleza maumivu yangu. -
3:03 - 3:09Kwa hivyo kisa hicho, nadhani, kikawa
kingumu sana kwake. -
3:09 - 3:16Na kisha akaamua kunielekeza kwenye
hospitali kubwa zaidi kwa huduma za ushauri. -
3:16 - 3:23Nikaenda na kufika pale wakanipa
mapokeo ya dharura. -
3:23 - 3:28Kwa hiyo nilipata timu ya madaktari na wauguzi.
Walikuja na kunichunguza. -
3:28 - 3:31Walinihoji na
nikawaambia kila kitu. -
3:31 - 3:39Na kisha wakasema wataenda kuchukua X-ray na kisha kufanya uchunguzi(scan) wa moyo wangu.
-
3:39 - 3:46Kwa hiyo walikuja na kunichukua ndani na kuchukua
X-ray mbili za sehemu ya kifua changu. -
3:46 - 3:52Walichukua sampuli za damu kutoka kwangu,
kwa kweli sampuli nyingi za damu, -
3:52 - 3:55kwa sababu walilazimika kufanya majaribio kadhaa.
-
3:55 - 4:02Kilichonishangaza ni, baada ya kuchunguza
mfululizo wa majaribio hayo yote waliyofanya, -
4:02 - 4:10waligundua kuwa hakuna kitu - kila kitu kiligeuka kuwa hasi.
-
4:10 - 4:14Jumamosi ijayo tungekuwa
na -
4:14 - 4:19tukio la mhadhara la 'Acha Mioyo Iamke'
nchini Uingereza. -
4:19 - 4:24Nilikuwa na bahati ya kupokea
kiungo ili nijiunge mtandaoni, -
4:24 - 4:27kwa hivyo nilikuwa nikitarajia.
-
4:27 - 4:31Na moyoni mwangu nilikuwa na imani.
-
4:31 - 4:39Nilifikiria, kama kisa hiki kimekuwa,
-
4:39 - 4:45kigumu sana kwa mwanadamu kufasiri,
nitakileta mbele za Mungu. -
4:45 - 4:48Najua lisilowezekana kwa mwanadamu
linawezekana kwa Mungu. -
4:48 - 4:53Jumamosi ilifika na nikajiunga.
Nilitarajia. -
4:53 - 5:03Nilijua kisa hiki kimekaidi maarifa ya matibabu
na hakitakaidi uwezo wa Mungu. -
5:03 - 5:09Kwa hiyo maombi yakaanza na
tukasikiliza shuhuda. -
5:09 - 5:15Kisha mtu wa Mungu alipokuja,
alipokuwa akiwaombea watu, -
5:15 - 5:20Nilianza kuona nguvu za Mungu
zikiwagusa watu. -
5:20 - 5:22Watu walikuwa wakijidhihirisha.
-
5:22 - 5:27Kweli Mungu alikuwa anatembea kwa nguvu
pale ukumbini. -
5:27 - 5:32Na alipokuwa akiwaombea watu,
maombi yangu yalikuwa moja tu. -
5:32 - 5:38Niliendelea kusema moyoni mwangu, 'Bwana, unapowagusa
wengine, usinipite. -
5:38 - 5:43Unapowatembelea wengine, tafadhali Bwana,
usinipite. -
5:43 - 5:51niko hapa. Najua umbali sio kizuizi kwa nguvu zako. Unaweza kunigusa.'
-
5:51 - 5:56Lakini mnajua, watu wa Mungu,
nilichogundua ni -
5:56 - 6:02kwamba hata kabla ibada
haijafikia hatua -
6:02 - 6:08ambapo mtu wa Mungu alijitokeza kuwaombea
watazamaji waliokuwa wameunganishwa mtandaoni, -
6:08 - 6:14Niligundua kuwa maumivu yalikuwa
yametoweka yenyewe. -
6:14 - 6:16Ndugu Chris alipokuja
kuwaombea watazamaji, -
6:16 - 6:21na akasema kwamba watu
wanapaswa kugusa sehemu hizo -
6:21 - 6:29ambapo walikuwa na maumivu au usumbufu,
wakati huo kulikuwa na maumivu kidogo sana -
6:29 - 6:35nami nikagusa na nadhani hiyo
ilitia muhuri uponyaji wote kwa ajili yangu. -
6:35 - 6:42Na baada ya hapo, nilihisi vizuri.
Usiku huo, nililala vizuri. -
6:42 - 6:45Siku iliyofuata ningeweza
kufanya mambo ambayo sikuweza kufanya. -
6:45 - 6:49Ningeweza kuinama.
Ningeweza kugeuka. -
6:49 - 6:53Siku ya Jumatatu, nilirudi kazini
na nilikuwa sawa. -
6:53 - 7:00Nilirejeshwa kikamilifu. Utukufu ni kwa Mungu.
Sasa niko huru kabisa! -
7:00 - 7:05Kama unavyoona,
sikuweza kusonga kama hii. -
7:05 - 7:07Sikuweza kufanya hivi kwa sababu
-
7:07 - 7:11maumivu yangekuwa makali sana
na kupenya hadi kifuani mwangu. -
7:11 - 7:14Sikuweza kusimama.
-
7:14 - 7:18Sasa naweza kuruka.
-
7:18 - 7:22Kwa hiyo niko huru kabisa
kwa utukufu wa Mungu! -
7:22 - 7:25Je, ulisikia maumivu yoyote wakati wa kufanya mazoezi?
-
7:25 - 7:30Hapana, hata kidogo. Niko huru kwa utukufu wa Mungu.
-
7:30 - 7:35Tafadhali, sasa endelea na ushirikishe
neno lako zuri la ushauri kwa watazamaji. -
7:35 - 7:42Tunahitaji kumtegemea Mungu,
na tunahitaji kutambua -
7:42 - 7:46ya kwamba yasiyowezekana kwa mwanadamu
yanawezekana kwa Mungu. -
7:46 - 7:51Hali yoyote ambayo inaweza kukujia,
usivunjike moyo. -
7:51 - 7:55Jua kuwa lililo gumu kwako,
-
7:55 - 8:00lisilowezekana kwa mwanadamu,
kwa Mungu linawezekana. -
8:00 - 8:07Mungu anapendezwa nasi kumkazia macho, kumaanisha kumtumaini.
-
8:07 - 8:13Kwa maana Maandiko Matakatifu yasemavyo:
'Bila imani hatuwezi kumpendeza Mungu.' -
8:13 - 8:19Mungu anaheshimiwa tunapomtegemea
, tunapomtumaini. -
8:19 - 8:25Kwa hivyo ushauri wangu ni, bila kujali hali,
haijalishi mazingira, -
8:25 - 8:27hakuna lisilowezekana
kwa Mungu. -
8:27 - 8:30Tumtegemee Mungu.
Tumtumaini Yeye. -
8:30 - 8:36Na tunapomtumaini Yeye,
atatujia. -
8:36 - 8:41Atatugusa, Atagusa
hali zetu na tutafanywa kuwa wakamilifu.
- Title:
- Maombi nchini Uingereza; Muujiza nchini NORWAY!
- Description:
-
Umbali sio kizuizi kwa nguvu za Mungu! Ivan alikuwa Norway alipojiunga na 'Acha Mioyo Iamke' - tukio la kwanza la umma la TV Ya Moyo Wa Mungu (God's Heart TV) nchini Uingereza - kupitia Zoom. Ndugu Chris alipokuwa akihudumia wengine maombi, alipokea uponyaji wake mwenyewe kutokana na maumivu makali ya kifua ambayo yalikuwa yamekaidi ujuzi wa kitiba. Kweli, kwa MUNGU hakuna lisilowezekana.
Ili kupokea maombi bila malipo kutoka kwa Ndugu Chris kupitia Zoom, wasilisha ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom
➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Kuwa Mshirika wa TV wa Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/partnership
➡️ Habari kuhusu Maombi ya Pamoja - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shirikisha ushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live - Video Language:
- English
- Team:
God's Heart TV
- Duration:
- 09:12
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Prayer in UK; Miracle in NORWAY! | |
![]() |
georgejbudeba edited Swahili subtitles for Prayer in UK; Miracle in NORWAY! |