Vimelea vya minyoo vinarudisha nyuma maendeleo ya mwanadamu. Hii ndiyo namna ya kuvitokomeza.
-
0:00 - 0:02Hawa ni minyoo.
-
0:02 - 0:05Si minyoo ambayo utaiona ikitambaa kwenye uchafu
-
0:05 - 0:07Hivi ni vimelea vya minyookuru.
-
0:07 - 0:09Wanaishi ndani utumbo wa mwanadamu.
-
0:09 - 0:12Kila mmoja wa minyoo hii huweza kukua hadi urefu wa inchi 12,
-
0:12 - 0:14na wapo 200 katika kopo hili kwa sababu fulani,
-
0:15 - 0:17kwa sababu hiyo ni idadi ambayo kwa kawaida utawakuta
-
0:17 - 0:19ndani ya tumbo la mtoto anayeugua.
-
0:19 - 0:22Maambukizi ya minyoo yamekuwapo kwa takribani ya maelfu ya miaka.
-
0:22 - 0:24Yamechangia katika matokeo ya baada ya vita,
-
0:24 - 0:26na kukinzana na afya ya mwanadamu kwa muda sana.
-
0:26 - 0:28minyookuru, safura,
-
0:28 - 0:30minyoo-mjeledi, kichocho:
-
0:30 - 0:33maambukizi kutoka katika vijidudu hivi husababisha maumivu na kukosa raha.
-
0:33 - 0:35Huiba virutubisho na kunyong'onyeza mwili.
-
0:35 - 0:37Hudumaza ukuaji wa kimwili na kiakili.
-
0:37 - 0:40Katika matukio mbalimbali, minyoo hawa huwa si wenye madhara makubwa,
-
0:40 - 0:42lakini cha kushangaza, hiyo ndiyo sababu mojawapo ya tatizo.
-
0:42 - 0:44Inamaanisha kwamba nchi nyingi
-
0:44 - 0:47hazihitajika kuweza kutoa kipaumbele cha matibabu yake.
-
0:47 - 0:48Na kuna madhara kwa jamii kutokana na hilo:
-
0:48 - 0:51watoto ambao hawapati huduma za dawa za kuua minyoo
-
0:51 - 0:53wana mahudhurio ya chini shuleni.
-
0:53 - 0:55Watu wazima ambao hukua bila kutumia dawa za kuua minyoo
-
0:55 - 0:58hawawezi fanya kazi kwa juhudi na huwa na kipato duni.
-
0:58 - 1:00Kitu ambacho minyoo hufanya, kihalisia,
-
1:00 - 1:01ni kuweka kikwazo cha uwezo wa uchapakazi.
-
1:01 - 1:05Hadi sasa, kuna watu bilioni 1.7 duniani walio katika hatari ya minyoo hii.
-
1:05 - 1:08Milioni mia sita kati yao wanaishi Afrika.
-
1:08 - 1:11Kwa kila dola inayowekezwa katika kupambana na kuondokana na minyoo,
-
1:11 - 1:15Afrika inapata hadi dola 42 katika faidiko la kiuchumi.
-
1:15 - 1:18Habari njema ni kwamba matibabu ya kuua minyoo ni rahisi mno.
-
1:18 - 1:21Kuanzia kidonge kimoja hadi vitatu vikitolewa mara moja au mbili kwa mwaka
-
1:21 - 1:24hutosha kabisa kumfanya mtoto kutoka kuwa na minyoo 200 hadi kutokuwa na mnyoo hata mmoja
-
1:24 - 1:26na kuwalinda na maambukizi yajayo.
-
1:26 - 1:29Katika jamii ambazo kuna uwepo mkubwa wa minyoo,
-
1:29 - 1:31matibabu yanaweza fanyika shuleni.
-
1:31 - 1:33Mchakato huu ni rahisi na wa haraka.
-
1:33 - 1:36Nchini Ethiopia, kwa mfano, hii inafanyika kwa watoto milioni 20
-
1:36 - 1:38ndani ya wiki chache tu.
-
1:38 - 1:40Dunia imetoka mbali
-
1:40 - 1:43katika kuwapatia dawa za minyoo watu wanaozihitaji,
-
1:43 - 1:45na serikali za nchi za Afrika zinataka kupata msukumo.
-
1:45 - 1:47Ni wakati sasa wa kuendana na malengo yao.
-
1:48 - 1:50Mradi wa END utashirikiana na serikali
-
1:50 - 1:54kuandaa mpango madhubuti wa kupunguza mzigo wa magonjwa yanayosababishwa na minyoo.
-
1:54 - 1:58Watafanya kazi pamoja kuhakikisha programu za kinga na tiba
-
1:58 - 1:59zinaweza kumpa huduma kila mtu.
-
1:59 - 2:01Mradi wa END una wazo lenye uthubutu:
-
2:01 - 2:06wanaamini kwamba sisi ni kizazi ambacho kitakomesha magonjwa yatokanayo na minyoo milele.
-
2:06 - 2:09Mpango si tu kuunda programu mpya kuanzia mwanzo,
-
2:09 - 2:12lakini kuzipa muamko zaidi juhudi za programu ambazo tayari zinaleta mabadiliko.
-
2:12 - 2:16Kwa kutathmini tatizo la namna gani minyoo husambaza magonjwa,
-
2:16 - 2:19mradi wa END umegundua sehemu tano muhimu ambazo wanaweza fanyia maboresho.
-
2:20 - 2:22Namba moja: matibabu yaliyo nafuu.
-
2:22 - 2:26Makampuni mengi ya kutengeneza madawa hutoa dawa za minyoo bure,
-
2:26 - 2:28hivyo mradi wa END unafanya kazi na washirika sahihi
-
2:28 - 2:29kusimamia utoaji wa dawa.
-
2:29 - 2:32Wataendelea kusimamia utoaji wa dawa
-
2:32 - 2:34katika jamii ambazo zipo katika hatari.
-
2:35 - 2:39Sasa wanaweza kufanya kwa chini ya zaidi ya senti 25 kwa mtoto katika mwaka mmoja.
-
2:39 - 2:42Namba mbili: kutazamia katika kinga.
-
2:42 - 2:45Mradi wa END unahamasisha washirika sahihi ili kuelimisha jamii
-
2:45 - 2:46katika usafi wa mazingira na usafi binafsi
-
2:46 - 2:49ili kuweza kubadili mienendo kama kuosha mikono
-
2:49 - 2:50na matumizi ya msalani,
-
2:50 - 2:53kuhakikisha kwamba watu hawapati tena maambukizi.
-
2:53 - 2:56Namba tatu: kuwekeza katika ubunifu.
-
2:56 - 2:58Mradi wa END umechangia katika kutokomeza minyoo
-
2:58 - 3:02kwa kuleta namna za kibunifu ambazo zinawalenga watu na kuwatibu.
-
3:02 - 3:04Watajaribu namna mpya za utoaji huduma,
-
3:04 - 3:06kulenga mazingira ambayo vimelea huweza kuishi
-
3:06 - 3:08na kushawishi mabadiliko ya mienendo.
-
3:08 - 3:11Namba nne: kusimamia na kufanya tathmini.
-
3:11 - 3:14Mradi wa END hukusanya taarifa za programu zote mara kwa mara
-
3:14 - 3:17ili kuweza kuboresha programu zaidi na zaidi kadiri muda unavyokwenda.
-
3:17 - 3:20Namba tano: kuongeza umilikishaji katika jamii.
-
3:20 - 3:22Katika hatua zote za mchakato,
-
3:22 - 3:25mradi wa END unafanya kazi na serikali na wadau katika jamii
-
3:25 - 3:29ili kuweza kuchangia michango ya kifedha kwa pamoja ili kuunga mkono juhudi za kuondokana na minyoo.
-
3:29 - 3:31Wamefanya kazi wa wahisani kutoka Afrika
-
3:31 - 3:34na viongozi wa makampuni katika juhudi hizi.
-
3:34 - 3:37Kuna fursa kubwa sana ya kufanya kazi pamoja kutengeneza namna mpya
-
3:37 - 3:41ya kuondoa ugonjwa kwa muongo unaofata na zaidi.
-
3:41 - 3:42Kiasi cha fedha ambacho mradi wa END unahitaji
-
3:42 - 3:45kitakwenda moja kwa moja katika utoaji wa matibabu ya minyoo
-
3:45 - 3:46kwa jamii ambazo zina uhitaji
-
3:46 - 3:50na kiasi kingine kitaenda katika uwezeshaji wa miradi
-
3:50 - 3:51kwa umilikishaji wa jamii.
-
3:51 - 3:55Kwa pamoja, hizi juhudi zitatengeneza programu za kukinga na kutibu
-
3:55 - 3:57ambazo zitakuwa madhubuti hadi miaka ijayo.
-
3:57 - 4:01Kama mradi huu utawezeshwa kifedha kwa miaka sita ijayo,
-
4:01 - 4:05makumi ya mamilioni ya watu wataweza pata matibabu ya minyoo.
-
4:05 - 4:09Kwa hilo, nchi zitaweza kuuondoa mzunguko wa maambukizi ya ugonjwa
-
4:09 - 4:10katika ngazi zote,
-
4:10 - 4:14na lililo muhimu zaidi, watu wataweza kuimarika zaidi
-
4:14 - 4:17katika afya ya kiakili, kimwili na mahusiano ya kijamii.
-
4:17 - 4:19Hebu fikiria uwezo utakao kuwepo
-
4:19 - 4:22pale watu wanapokoma kupata wasiwasi wa jambo hili
-
4:22 - 4:25na kuweka nguvu zao katika mambo kama haya.
-
4:25 - 4:27(Wanafunzi wakipaza sauti)
-
4:27 - 4:30(Wakipiga makofi na kuimba)
-
4:30 - 4:33(Wakishangilia)
- Title:
- Vimelea vya minyoo vinarudisha nyuma maendeleo ya mwanadamu. Hii ndiyo namna ya kuvitokomeza.
- Speaker:
- Ellen Agler
- Description:
-
Vimelea vya minyoo vimekuwepo tangu maelfu ya miaka, kusababisha magonjwa ambayo yanapunguza uwezo wa mwanadamu. Lakini leo, tiba bora ya kuondokana nayo inahitaji vidonge vichache tu, vikitumika mara moja au mbili kwa mwaka. Ikiwa ni watu bilioni 1.7 walio katika hatari ya maambukizi, Ellen Agler na timu yake ya mradi wa END wanatazamia dunia isiyo na ugonjwa unaosababishwa na minyoo. Jifunze ni namna gani wanafanya juhudi katika kupunguza gharama za matibabu, kuboresha kinga, kusaidia serikali na kusaidia uongozi katika jamii. Mpango huu wenye uthubutu ni moja mradi wa The Audacious, mradi ulioanzishwa na TED ili kuhamasisha na kuchangia katika mabadiliko ulimwenguni.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 04:48
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Parasitic worms hold back human progress. Here's how we can end them | |
![]() |
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Parasitic worms hold back human progress. Here's how we can end them | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Parasitic worms hold back human progress. Here's how we can end them | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Parasitic worms hold back human progress. Here's how we can end them | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for Parasitic worms hold back human progress. Here's how we can end them |