-
Hebu tufanye maswali ya
-
kukokotoa milinganyo.
-
Tuchukulie tuna mlinganyo huu, 1/3 jumlisha A
-
ni sawa na 5/3.
-
Je, thamani ya A ni ngapi kwenye mlinganyo?
-
Kama nina 1/3 jumlisha A, je A inatakiwa kuwa ngapi
-
ili tukiijumlisha kwa 1/3 iwe sawa na 5/3?
-
Kuna njia nyingi za kufanya hii,
-
na hiki ni kitu cha kufurahisha kuhusu mlinganyo
-
na hakuna njia moja ya kukokotoa.
-
Hivyo ngoja nifikirie,
-
njia nyepesi ya kutumia.
-
Na kabla sijafanya chochote, unaweza
-
kusubirisha video, na ufanye mwenyewe.
-
Hivyo nachotakiwa ni kuwa na A
-
upande mmoja wa mlinganyo.
-
Kwa kuwa A ipo tayari upande wa kushoto,
-
tuone kama nitaweza kuendelea kuiweka upande wa kushoto,
-
hivyo naiondoa 1/3.
-
Vizuri, njia rahisi ya kuiondoa
-
hii 1/3 ni kutoa 1/3 kutoka upande wa
-
kushoto wa mlinganyo.
-
Siwezi kutoa
-
upande wa kushoto wa mlinganyo peke yake.
-
Kama 1/3 jumlisha A ni sawa na 5/3,
-
na kama nikitoa 1/3 kutoka upande wa kushoto tu,
-
hivyo haiwezi kuwa sawa.
-
Hivyo upande huu utakuwa pungufu ya 1/3,
-
endapo upande huu hautobadilika.
-
Hivyo basi upande wa kushoto utakuwa
-
pungufu ya 5/3.
-
Kwa hiyo ili kupata usawa, nitakachokifanya
-
upande wa kushoto nitakifanya upande wa kulia pia.
-
Hivyo nitatoa 1/3 pande zote.
-
Na kama nikifanya hivyo, upande wa kushoto,
-
1/3 toa 1/3, ndiyo maana
-
nimetoa 1/3 ili kuondoa 1/3,
-
na nimebakiwa na A ni sawa na 5/3 toa 1/3,
-
5/3 toa 1/3,
-
toa 1/3 , tutapata ngapi?
-
Nina tano ya kitu hapa, kwenye hili swali nina 5/3,
-
ninatoa kwa 1/3.
-
Hivyo nitabakiwa na 4/3.
-
Hivyo nitaandika A ni sawa na 4/3.
-
Unaweza kuhakikisha kama ni sahihi.
-
1/3 jumlisha 4/3 ni sawa na 5/3.
-
Hebu tufanye mfano mwingine.
-
Tuchukulie tuna mlinganyo huu, K toa nane
-
ni sawa na 11.8.
-
Kwa mara nyingine, natafuta thamani ya K.
-
Nina K upande wa kushoto.
-
Sihitaji kuwa na hii, toa nane hapa.
-
Hivyo ili kuondoa hii nane, hivyo tuongeze nane
-
upande wa kushoto.
-
Hivyo, kama nafanya hivi upande wa kushoto,
-
nitafanya hivyohivyo upande wa kulia.
-
Hivyo tunaongeza nane pande zote.
-
Upande wa kushoto, unatoa nane
-
na pia unajumlisha nane.
-
Hii inaisha,
-
na unabakiwa na K.
-
Na upande wa kulia, 11.8 jumlisha nane.
-
Vizuri, 11 jumlisha nane ni 19, itakuwa 19.8.
-
Na tumemaliza,
-
Unaweza kuhakikisha kama umepata jibu sahihi.
-
19.8 toa nane ni 11.8.
-
Hebu tufanye nyingine, hii inavutia.
-
Sawa, tuchukulie nina 5/13 ni sawa na
-
T toa 6/13.
-
Vizuri, hii inavutia kwa sababu sasa nina mtajo
-
upande wa kulia.
-
Hivyo naiacha hapa.
-
Tuone kama tunaweza kutafuta thamani ya T kwa kuondoa
-
namba yoyote upande wa kulia.
-
Na kama tulivyofanya awali, kama natoa 6/13,
-
kwa nini nisiijumlishe?
-
Kwa nini nisijumlishe 6/13?
-
Siwezi kufanya hivyo upande wa kushoto.
-
Hizi pande mbili hazitakuwa sawa,
-
nitafanya hivyo upande wa kulia kama ninataka
-
kupata usawa.
-
Hivyo nini kitatokea?
-
Nini kitatokea?
-
Upande wa kushoto nina
-
ngoja niache nafasi kidogo,
-
nina 5/13 jumlisha 6/13,
-
jumlisha 6/13 ni sawa na ,
-
ni sawa na
-
Nilitoa 6/13, sasa najumlisha 6/13.
-
Hizi zitatupatia sifuri.
-
6/13 toa 6/13 inabaki sifuri, hivyo umebakiwa na T.
-
Hivyo T ni sawa na hii.
-
Kama nina 5/13 na najumlisha na hii 6/13,
-
Nitapata 11/13.
-
Hivyo hii itakuwa 11/13 ni sawa na T,
-
au naweza kuiandika kwa njia nyingine.
-
Naandika T ni sawa na 11/13.